Psalms 78:34-37

34 aKila mara Mungu alipowaua baadhi yao,
waliosalia walimtafuta,
walimgeukia tena kwa shauku.
35 bWalikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao,
kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.
36 cLakini walimdanganya kwa vinywa vyao,
wakisema uongo kwa ndimi zao,
37 dmioyo yao haikuwa thabiti kwake,
wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
Copyright information for SwhNEN